Mikakati yawekwa kuyakabili magenge ya kihalifu Kwale

 

Idara ya polisi kaunti ya Kwale inaendeleza mikakati ya kuyakabili magenge ya kihalifu yanayowahangaisha wenyeji wa kaunti hiyo hususan wale wanaoishi kwenye mpaka wa kaunti hiyo na Mombasa.
Kwa mujibu wa idara hiyo,siku za hivi karibuni magenge ambayo yamekuwa yakiwahangaisha wakaazi Mombasa yameingia kwenye kaunti ya Kwale kupanga njama za kutekeleza uvamizi.
Aidha, imebainisha kuwa magenge hayo hutumia pikipiki kuwahangaisha wafanyibiashara na wakaazi kwa jumla.
Kamishna wa kaunti hiyo, Karuku Ngumo amewataka wenyeji wa Kwale kupiga ripoti mara moja wakati ambapo kunatekelezwa uhalifu au wakati ambapo wamekisia kusikia kuhusiana na njama za uhalifu.
Ngumo amesema kuwa ni kupitia ushirikiano kati ya wenyeji na idara ya polisi ndipo magenge hayo yataweza kukabiliwa kikamilifu.
Haya yamejiri huku vijiji mbalimbali eneo la Ngomeni vikishuhudiwa visa vya watu kuuawa kwa kukatwakatwa na watu wasiojulikana.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.