Mechi za kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya (EURO 2020) zimeendelea jana

Mechi mbalimbali za kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya (EURO 2020) zimeendelea jana katika viwanja tofauti barani humo, Kundi A Uingereza imeimimia mvua ya magoli Kosovo kwa kuifunga 5-3, huku Jamhuri ya Czech ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Montenegro, katika kundi B, vijana wa Ureno wameifundisha Lithuania namna soka linavyochezwa kwa kuibamiza magoli 5-1, huku Serbia ikiibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Luxembourg. Na kundi H Albania imeibuka na ushindi wa 4-2 dhid ya Iceland, huku Ufaransa wakiwafunga Andorra kwa mabao 3-0, nao Uturuki wameonyesha ubabe wao kwa Moldova kwa kuwapa kichapo cha goli 4-0.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.