MARTHA KOOME ASEMA IDARA YA MAHAKAMA IMEJIANDAA

Jaji mkuu nchini Martha Karambu Koome amesema idara ya mahakama imejiandaa kukabiliana na kesi za mizozo ya uchaguzi ambayo huenda ikaibuka kabla na hata baada ya uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kuandaliwa mwaka ujao wa 2022.
Kwenye taarifa yake akiwa kaunti ya Mombasa Koome amesema tayari majaji wa mahakama kuu nchini wanaendelea na hamasa ya namna ya kutatua kesi za aina hiyo kulingana na sheria za katiba nchini.
Wakati uo huo jaji mkuu huyo amesema kuwa ujenzi wa mahakama kuu ya Mombasa uko karibu kukamilika na jengo hilo linatarjiwa kufunguliwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo ili kuwahudumia wananchi .

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.