MALKIA STRIKERS WAPOTEZA KOMBE DHIDI YA CAMEROON

Mipango ya Malkia Strikers ya Kenya ya kubeba kombe la African Nations women’s Volleyball Championships kwa mara ya 10 iliangukia pakavu baada ya timu hiyo kuruhusu kipigo dhidi ya bingwa mtetezi Cameroon katika uga wa Kigali Arena Rwanda Jumapili Septemba 20.

Malkia Strikers ambao walipoteza seti mbili za kwanza kwa alama 25-21 na 25-23 kabla ya kupata ushindi kwenye seti ya 3 kwa alama 25-15 hawakuweza kustahimili moto wa timu ya Cameroon kwenye seti ya nne na ya mwisho hivyo kulalishwa kwa alama 25-23.

Hata hivyo Sharon Chepchumba alitajwa kuwa mvamizi bora baada ya kuweka kimiani pointi 21 ila mchango wake haukuweza kufua dafu kuwapa ushindi warembo wa mkufunzi Paul Bitok.

Vipusa hao Kenya walifuzu fainali za michuano hiyo baada ya kuzamisha Morocco kwa seti tatu bila jawabu (3-0) kwenye nusu fainali.

Malkia walinyuka Morocco alama 25-12 kwenye seti ya kwanza, alama 25-21 katika seti ya pili na kumalizia udhia kwa alama 25-11..

Kwa kufuzu kuingia fainali Kenya ilijikatia tiketi ya kushiriki michuano ya Mabingwa wa Dunia itakayoandaliwa na Netherlands pamoja na Poland.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.