MAHAKAMA YATUPILIA MBALI MATUMIZI YA KADI ZA HUDUMA NAMBA

Mahakama kuu imetupilia mbali matumizi ya kadi za huduma Namba nchini.
Akitoa uamuzi huo Jaji Jairus Ngaa amesema wamebaini kuwa serikali haikufanya uchunguzi na kufuata taratibu zilizohitajika katika kubuni kadi hizo.
Kutupiliwa mbali kwa kadi hizo kunajiri baada ya kundi moja la wanaharakati kuwasilisha kesi mahakamani likihoji usalama wa maelezo ya wakenya yaliyotolewa wakati wa usajili.
Wakenya wamekuwa wakiamuriwa kuchukua kadi hizo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *