MAHAKAMA YA ICJ YATOA UAMUZI

Mahakama ya kimataifa imetoa uamuzi na kuratibisha mpaka mpya katika eneo linalozozaniwa kati ya Kenya na Somalia.

Kwenye uamuzi uliotolewa katika makao makuu ya mahakama hiyo jijini Hague Uholanzi, Mahakama hiyo imesema kuwa hakukuwa na makubaliano yoyote kati ya mataifa hayo mawili kuhusu mpaka huo. Majaji 11 kati ya 15 walifika mahakamani kutoa uamuzi unaohusu mzozo wa mpaka huo wa baharini, mgogoro uliochukua miaka saba mahakamani.

Wawakilishi wanne kutoka Somalia walikuwepo katika ukumbi wa mahakama na upande wa Kenya hakukuwa na mwakilishi kwani ilikuwa imetangaza kuwa haitafuata uamuzi wowote ambao utatolewa na mahakama hiyo ya ICJ.

Uamuzi huo uliposomwa hakuna upande wowote uliopata ulichotarajia huku mahakama hiyo ikiweka mpaka ulioko katikati ya maeneo ambayo mataifa ya Kenya na Somalia yalikuwa yanadai.

Majaji wa mahakama hiyo wakisema kuwa hakuna makubaliano yoyote kati ya mataifa hayo kuhusu eneo linalozozaniwa.

Mahakama hiyo ilipuzilia mbali madai ya Somalia kuwa Kenya ilivunja sheria za kimataifa kwa kuendeleza shuguli zake katika eneo linalozozaniwa.

Mataifa haya mawili yanazozania eneo la bahari Hindi lililo na upana wa maili 30,000 ambalo lina unatajiri wa mafuta na gesi na eneo ambalo Wavuvi kutoka Kenya wanategemea samaki kutoka eneo hilo kujikimu kimaisha.

Mzozo huo unachochewa zaidi na tafsiri tofauti za ramani ya Afrika katika fuo za bahari Hindi na kilichosalia kwa sasa ni kuona ni hatua hani itachukuliwa na Kenya hata baada ya kutangaza kuwa haitambui wala kutii uamuzi wa mahakama hiyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.