MAENEO YA WAVUVI KUVULIA SAMAKI ENEO LA WATAMU YAVUNJWA

Mwenyekiti wa usimamizi wa fuo za bahari BMU huko Watamu kaunti ya Kilifi Athman Mwambire analalamikia maeneo ya wavuvi ya kuvulia samaki pamoja na sehemu za biashara  kuanza kuchukuliwa na Mabwenyenye.

Mwambire akizungumza na meza yetu ya habari anasema kwamba hali hiyo itaathiri kwa kiwango kikubwa shughuli za uvuvi sambamba na biashara kwani maeneo hayo ya ufuo yanatumika na wafanyabiashara ili kuendeleza biashara zao kwa ajili ya kujipatia mapato.

Kwa mujibu wa Mwambire ameitaja hali hiyo kuwa inaweza kusababisha ukosefu wa usalama pamoja na kuibua chuki.

Mwambire anadai kuwa waliandaa mazungumzo na vitengo husika lakini licha ya hayo vibanda vikabomolewa.

Sasa ametoa wito kwa wizara husika pamoja na serikali zote mbili kuwashirikisha wahusika kabla ya kutekeleza ubomozi wowote.

Kisa hicho cha kuvunjwa kwa vibanda kilitokea katika sehemu ya Sun Palm eneo hilo la Watamu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.