MABATI ROLLING MILLS YAFUNGUA TAWI JIPYA HUKO VOI KAUNTI YA TAITA TAVETA

Mhandisi mkuu wa kampuni ya Mabati Rolling Mills Paul Omondi amesema wanaendeleza mikakati kuhakikisha wanawaelimisha Wakenya kuhusu umuhimu wa kununua mabati ambayo yanatengenezwa hapa nchini.

Akizungumza huko Voi katika kaunti ya Taita Taveta, katika ufunguzi wa tawi jipya eneo hilo la Voi, Mhandisi Omondi amesema wakenya wanapaswa kuthamini bidhaa ambazo zinatengezwa hapa nchini na kupitia hamasa ambazo wanazitoa, wananchi wataweza kufahamu mabati ambayo yanafaa katika ujenzi.

Omondi amesema kupitia tawi hilo la Voi, wafanyabishara wataimarika kibiashara na pia eneo la Voi kuimarika kiuchumi.

Ni kauli ambayo imeungwa mkono na Mkurugenzi wa Mabati Rolling Mills Dipti Mohanty na kuwataka Wananchi kuwa makini wanaponunua mabati katika baadhi ya maduka kwani kuna baadhi ya wafanyabiashara  ambao wanauza mabati ghushi.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *