Lamu | Wanawake wanatumiwa kuendeleza biashara ya dawa za kulevya

Imebainika kuwa baadhi ya wanawake katika kaunti ya Lamu wanatumiwa kuendeleza biashara haramu ya dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa baraza la viongozi wa dini mbali mbali CICC Mohammed Abdulkadir ni kuwa maafisa wa KDF wanakosa kuwakagua kina mama hali ambayo imekuwa ikichangia kwa wao kutumiwa katika kusafirisha mihadarari maeneo mbali mbali hasa katika ukanda huu wa pwani.

Abdulkadir sasa anasema ili kudhibiti hali hiyo ni sharti serikali iongeze maafisa wa kutosha wa usalama katika kaunti hiyo ili kusaidia kuwakagua abiria ambao wanaingia na kutoka katika kisiwa cha Lamu.

Kiongozi huyo wa kidini amesema ikiwa hilo halitashughulikiwa kwa haraka idadi ya vijana wanaotumia dawa za kulevya huenda ikaongezea kwa kiwango kikubwa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.