Kwale | Serikali yatakiwa kujengea shule ya wasichana ya Kwale jumba la mankuli

Serikali kupitia wizara ya elimu imeombwa kuweka mikakati ya ujenzi wa jumba la Maankuli kwa wanafunzi wa shule ya wasicahana ya Kwale.

Wakitoa wito huo mmoja wa wanachama wa bodi ya kusimamia raslimali za mafuta nchini Zainab Chidzuga amemtaka waziri wa elimu nchini Prof. George Magoha kuwahusisha wadau mbali mbali wa elimu katika kaunti hiyo kuhakikisha ujenzi wa ukumbi huo unakamilishwa kwa muda ufaao kabla ya kufunguliwa kwa muhula wa tatu kwa shule zote nchini tarehe 2 mwezi wa Septemba mwaka huu.

Ukumbi huo unadaiwa kuporomoka wanafunzi wa shule hiyo walipokuwa wakila chakula cha mchana ila hakuna mwanafunzi ambaye alijeruhiwa kutokana na kisa hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.