Kwale | Mimba za utotoni mmezichangia wenyewe wazazi~Magoha

Waziri wa elimu nchini Prof. George Magoha, amewataka wazazi katika kaunti ya Kwale kutenga muda zaidi ili kukaa na watoto wao na kuwaelekeza katika maadili yaliyo mema.

Akizungumza katika kaunti ya Kwale kwenye maadhimisho ya kitaifa ya siku ya vijana mjini Kwale amesema kuwa wazazi wamechangia kwa asilimia kubwa kushuhudiwa kwa visa vya mimba za mapema kwa kuwa hawana muda na watoto wao.

Aidha, ametoa tahadhari kwa jamii kuwaoza wanao wa kike kwani hatua hiyo huwa inapelekea kwa mtoto wa kike kukumbwa na matatizo ya afya yanayotokana na afya ya uzazi.

Hata hivyo kwa upande wake gavana wa kaunti hiyo Salim Mvurya amepinga mapendekezo ya baadhi ya viongozi kuhusu kurudishwa kwa sekta ya afya kwa serikali kuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.