Kwale | Asilimia kubwa ya wanawake wanaojiuza kingono Kwale wako kwenye hatari ya kuambukizwa UKIMWI

Imebainika kuwa idadi kubwa ya wanawake wanaojihusisha na biashara ya ngono kaunti ya Kwale wako katika hatari ya kuambikizwa ugonjwa wa ukimwi.

Ni kauli yake mshirikishi wa kituo cha kurekebisha tabia cha waraibu wa dawa za kulevya ,Teens Watch Caroline Omondi ambaye anasema msukumo wa dawa za kulevya ndio unaowapelekea wanawake hao kujihusisha na biashara ya ngono.

Ni usemi ambao imeungwa mkono na afisa wa maswala ya sheria katika shirika la Reach Out Centre Trust Mwinyi Abbas anayedai kuwa changamoto zinazowakumba waraibu wa kike ni nyingi zikilinganishwa na zile za jinsia ya kiume.

Abbas amesema tayari wameweka mikakati ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi miongoni mwa wanawake walioathirika na utumizi wa dawa za kulevya.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.