Kwaheri Ubelgiji, Mbwana Samatta kutua Uingereza

Duru za kuaminika zinasema kwamba, mshambuliaji wa kimataifa wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta anatarajia kuondoka nchini Tanzania kati ya kesho kutwa Ijumaa au Jumatatu kuelekea nchini Uingereza kukamilisha mipango yake ya kucheza ligi kuu nchini humo.

Samatta ambaye ni nahodha wa Taifa Stars, anatajwa kugombewa na Klabu ya Leicester City na Middlesbrough zinazoshiriki Ligi Kuu England.

Samatta ambaye aliiongoza Taifa Stars kwenye michuano ya Afcon inayoendelea nchini Misri na kuishia hatua ya makundi, anatakiwa na timu hizo kwa dau lililotajwa pauni milioni 12 ambazo ni zaidi ya bilioni 32 za Kitanzania.

Mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita alifunga mabao 23, katika Ligi Kuu ya Ubelgiji, amekuwa akitakiwa na timu nyingi barani Ulaya hasa England ambapo ukiziondoa Leicester na Middlesbrough, pia Aston Villa iliyopanda daraja kushiriki Premier nayo inamuhitaji.

Taarifa za uhakika kutoka katika chanzo cha kuaminika zinaeleza kuwa mshambuliaji huyo anatarajia kuondoka nchini keshokutwa Ijumaa au Jumatatu ya wiki ijayo kutokana na visa yake kukamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.