KUNA MIPANGO YA KUMVUA KILEMBA CHA UKUFUNZI OLE GUNNAR – PHIL NAVILLE

Aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Manchester United, Phil Naville, amesema kushindwa kwa klabu hiyo ya mashetani wekundu dhidi ya mabingwa wa Bundesliga RB Leipzig kwenye mechi ya ligi ya mabingwa ya ulaya ni njama fiche ya kumbandua kocha Ole Gunnar Solskjaer.

Kwa mujibu wa Naville, ambaye aliwahi kucheza na Ole Gunnar, ni kwamba kuna mbinu fiche ya kumng’oa Solskjaer klabuni Manchester United. Raia huyo wa Uingereza amesistiza kwamba kutemwa nje kwa Mashetani wekundu katika hatua ya makundi sio pigo la kustaajabisha.

United walikuwa kwenye mchakato wa kusaka pointi moja tu wakati wa ziara yao nchini Ujerumani mnamo Jumanne, Disemba 8 usiku, ili kujikatia tiketi ya kufuzu kwa raundi ya muondoano wa mtanange huo wa bara Ulaya.

Hata hivyo, ilisalia ndoto huku Leipzig, ambao walishiriki nusu fainali msimu uliopita wakisukwa upya na kufuzu kwa kuwazima Mashetani Wekundu.

Miamba hao wa Bundesliga walianza mechi hiyo ya Kundi H kwa matao ya juu, huku Angeliño akifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya pili ya mchezo, kombora lake likimshinda maarifa David de Gea.

Amadou Haidara alisawazisha bao hilo dakika kumi baadaye akimalizia vyema krosi ya Angeliño.

Wenyeji walidhania kuwa walipiga msumari wa mwisho kwenye mchezo huo lakini teknolojia ya VAR ilifuta bao la Orban. United walirejea mchezoni baadaye lakini walishindwa kuonja wavu licha ya kutawala dakika 15 za mwisho za awamu ya kwanza.

Justin Kluivert, alitoka benchi na kubadilisha matokeo kuwa 3-0 kunako dakika ya 69 kabla ya Bruno Fernandes kufungia United bao la kwanza kupitia mkwaju wa penalti.

Klabu ya Ligi Kuu iliendelea kukaza kamba huku juhudi zao zikizaa matunda katika dakika ya 83 wakati Pogba alifunga bao la pili akitumia kichwa kupachika mpira wavuni baada ya mpira kumgonga Harry Maguire.

Jaribio la mwisho la United liligonga mwamba huku wenyeji wakishikilia ushindi wao. Vijana wa Ole Gunnar Solskjaer wamebanduliwa kwenye Champions League na sasa wanajiunga na Arsenal na Tottenham Hotspur katika mkondo wa pili wa mashindano hayo.

1 thought on “KUNA MIPANGO YA KUMVUA KILEMBA CHA UKUFUNZI OLE GUNNAR – PHIL NAVILLE”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.