KRU YAAGIZA WANARAGA WOTE WACHANJWE LA SIVYO WASISHUKE DIMBANI

Wachezaji wote ambao hawajapokea chanjo ya covid 19  hawataruhusiwa kushiriki katika mechi za ligi kuu ya Kenya mchezo wa raga.

Muungano wa raga nchini ulichapisha sera ya chanjo siku ya Jumanne (23 November 2021) huku vilabu vikiwa na uamuzi wa kuchukua hatua kwa wachezaji ambao hawatapokea chanjo hiyo.

Mapema mwaka huu serikali ilitoa chanjo kwa wachezaji wote kama sehemu ya hatua salama ambazo zineruhusu kurejea kwa shughuli za michezo.

Utoaji huo pia uliwalenga wakufunzi  na wafanyikazi wengine ila serikali haikueleza bayana iwapo itawafungia nje wale walioamua kutochanjwa.

Kanuni hii ya Kenya Rugby Union kuhusu Covid 19 inajiri siku chache baada ya agizo la kuwa lazima wakenya waonyeshe uthibitisho wa kupokea chanjo ya Covid 19 kufikia Disemba 21 2021) ili kupata huduma za umma.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.