Kombe la Carabao | Bournemouth uso kwa uso na Manchester City

Sasa ni rasmi kwamba klabu ya Bournemouth watamenyana na Manchester City kwenye kivumbi cha kombe la Carabao baada ya kuwalaza Crystal Palace 11-10 kupitia mikwaju ya penalti kwenye raundi ya pili ya kipute hicho kufuatia ya kuambulia sare tasa mwishoni mwa dakika 90.

Ushindi wa Bournemouth uliwakatia tiketi ya kuchuana sasa na mabingwa watetezi Manchester City kwenye raundi ya tatu wiki ijayo.

Baada ya wachezaji wote 20 (isipokuwa makipa), kufunga penalti zao, mlinda-lango Wayne Hennessey aliudaka mkwaju wa kipa Asmir Begovic wa Bournemouth kabla yay eye mwenyewe kuupaisha mkwaju wake juu ya mlingoti.

David Brooks alifunga mkwaju wake wa pili wakati wa kuchanjwa kwa penalti huku Begovic akipangua kombora la Luka Milivojevic kwa upande wa Bournemouth na kuwapa fursa ya kusonga mbele.

Bournemouth walitamalaki mchezo, wakawazidi maarifa wapinzani wao katika takriban kila idara na kuwaelekezea makombora 17 yaliyolenga shabaha. Palace walifanya majaribio manne pekee langoni pa Bournemouth walioshushwa daraja kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mwishoni mwa msimu wa 2019-20 baada ya kipindi cha miaka mitano.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.