KIWANDA CHA PAMBA KUJENGWA ENEO LA KINONDO KAUNTI YA KWALE

Katibu katika wizara ya viwanda na biasahara nchini Ali Noor Ismail amesema serikali kuu kupitia wizara hiyo imezindua rasmi mradi wa ujenzi wa kiwanda cha pamba eneo la Kinondo kaunti ya Kwale.
Amesema ni kiwanda ambacho kitagharimu kima cha shilingi milioni 70 na kitawanufaisha kwa kiwango kikubwa wakulima wa pamba kwa kile ambacho amesema watapata soko la kuuza mazao yao.
Ameongeza kwamba serikali kuu tayari imefufua kiwanda cha kutengeneza nguo cha Rivertex hivyo ujenzi wa kiwanda hicho kutasaidia wakulima kuuza mazao yao ya pamba.
Aidha Gavana wa kaunti hiyo Salim Mvurya ametaka mradi huo kuungwa mkono ili kuboresha kilimo hicho cha pamba ambacho kimekuwa kikifanya vyema katika miaka ya nyuma eneo hilo.

1 thought on “KIWANDA CHA PAMBA KUJENGWA ENEO LA KINONDO KAUNTI YA KWALE”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.