KIMENUKA, MASHABIKI WATAKIWA KUVAA BARAKOA KUTAZAMA SIMBA NA YANGA WAKIKWARUZANA

Mashabiki wa soka wanaendelea kuwasili Kigoma nchini Tanzania, kuelekea mchuano wa fainali ya Kombe la Shirikisho la soka la Tanzania, TFF, baina ya Yanga na Simba, wametakiwa, kuvaa barakoa na kunawa mikono pamoja na kuchukua tahadhari nyingine ili kujikinga na maradhi ya Virusi vya Covid-19.

Yanga itapimana nguvu dhidi ya Simba siku ya Jumapili Julai 25 2021 katika dimba la Ziwa Tanganyika ukiwa ni mchezo wa kwanza baina ya miamba hao wa soka kupigwa mkoani Kigoma katika mashindano ya ASFC.

Kwa mjibu wa mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ni kwamba tahadhari hiyo sio tu kwa watakaoingia uwanjani hata wataokuwa wanaangalia mpira kwenye televisheni mitaani nao wavae barakoa na kunawa mikono kwa maji tiririka.

Simba na Yanga zimewasili mkoani hapo tangu Jana Alhamisi wakifanya maandalizi ya mwisho kwaajili ya mtanange huo, utakaopigwa kuanzia saa tisa na nusu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.