Kilifi | Zaidi ya visa 30 vya dhulma kwa watoto vimehusisha walimu

Huku visa vya dhulma dhidi ya watoto kanda ya pwani vikitafutiwa suluhu la kudumu sasa shirika la Social Justice Working Group ambalo ni la kutetea haki za kibinadamu limetaja visa hivyo kuongezeka kaunti ya Kilifi.

Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari mwenyekiti wa shirika hilo Simon Kazungu amehoji kuwa zaidi ya visa 30 vya dhulma dhidi ya watoto katika kaunti ya Kilifi vimehusisha walimu.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa wakati umefika wa kusitishwa kwa kuwa watoto wengi wameathiriwa pakubwa kisaikolojia.

Ameongezea kuwa watashirikiana na wadau mbali mbali pamoja na watetezi wa haki za watoto ili kuhakikisha kuwa haki za watoto zinalindwa vilivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.