Kilifi | Viongozi wakinzana na msimamo wa mbunge wa Malindi Bi. Aisha Jumwa

Viongozi mbalimbali katika kaunti ya kilifi wamekinzana na msimamo wa kisiasa wa mbunge wa Malindi, Aisha Jumwa hasa wa kukiasi chama cha ODM.

Wakiongozwa na mbunge wa Rabai William Kamoti wamedai Aisha Jumwa analenga kuwapotosha wakazi wa wadi ya Ganda na kumtaja mbunge huyo wa malindi kuwa mbinafsi.

Kulingana na Kamoti viongozi wasio na ajenda wanapaswa kutopewa kipau mbele katika nyadhifa za uongozi.

Kwa upande wake mbunge wa Magarini Michael Kingi ameunga mkono kauli ya Kamoti akisema kiongozi huyo amekosa mwelekeo licha kuwa mmoja kati ya wale waliondani ya chama cha ODM.

Naye mbunge wa Ganze Teddy Mwambire amesema Jumwa ni tapeli wa kisiasa, baada ya wabunge wote wa kilifi kumtetea wakati alipokuwa na migogoro na chama cha ODM.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.