Kilifi | Serikali ya kaunti ya Kilifi kuajiri wajuzi wa kukabiliana na visa vya watu kuzama baharini

Mwenyekiti wa chama cha maswala ya baharini BMU eneo la Malindi kaunti ya Kilifi Mohammed Abdalla Shekeli amesema serikali ya kaunti ya Kilifi imeajiri watu ambao wamepewa mafunzo ya kukabilina na visa vya watu kuzama baharini ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa mara kwa mara.

Akizungumza na meza yetu ya habari Shekeli amehoji kuwa kuna boti la uokozi ambalo limenunuliwa na serikali ya kaunti hii ili kurahisisha shughuli za kuwaokoa wanaozama kwenye bahari.

Ameitaka serikali kuu kuimarisha vifaa vya kisasa ambavyo vinaweza vikatumika baharini katika kumtambua kwa urahisi yule ambaye amezama baharini na anahitaji msaada wa dharura.

Hata hivyo, ametoa wito kwa asasi husika za kiusalama kuhakikisha zinaboresha mbinu zake katika kukabiliana na visa vya watu kuzama baharini.

Kauli yake inajiri siku chache baada ya gari moja dogo kuzama katika kivuko cha feri cha Likoni kaunti ya Mombasa ambapo mama pamoja na mtoto wake walizama maji hali ambayo imechukua masaa mengi kupata miili hiyo kutokana na ukosefu wa vifaa  maalum vya kuondoa miili hiyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.