Kilifi | Marufuku ya uchomaji makaa, kikwazo kwa wakaazi wa Magarini

Marufuku iliyotolewa na serekali ya ukataji wa miti na uchomaji wa makaa umetajwa kuwaathiri baadhi ya wakaazi wa gatuzi dogo la Magarini kaunti ya Kilifi.

Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya wazazi kutoka kijiji cha Mtsangamali kaunti ndogo ya Magarini wamesema kwamba tangu marufuku hiyo ilipoanza kutekelezwa wamekuwa wakipata changamoto katika kulipa karo za wana wao.

Kulingana na mzee wa mtaa wa eneo hilo Gilbert Thoya ni kwamba wazazi wengine eneo hilo wamekuwa wakitegemea biashara ya uchomaji wa makaa na marufuku hiyo imewakosesha kipato wazazi hao.

Aidha Thoya ameitaka serekali ya kaunti ya Kilifi kuja na njia mbadala ya kuwainua kiuchumi wakaazi kwani iwapo hali hiyo itaendelea huenda ikapelekea wanafunzi wengi kutohudhuria masomo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.