Kilifi | Mahakama kuandaa mkutano wa hamasa kwa umma Mayungu, mjini Malindi

Idara ya mahakama inatarajiwa leo kuandaa mkutano na umma katika soko la Mayungu mjini Malindi kaunti ya Kilifi.

Afisa wa kurekebisha tabia katika idara hiyo Linda Kumbu amesema mkutano huo unanuia kuhamasisha umma kuhusu huduma zinazopatikana mahakamani.

Aidha, umma utapatiwa nafasi ya kuwasilisha changamoto wanazopata katika kupata huduma za mahakama. Kumbu ameongeza kuwa kitengo cha urekebishaji tabia ni muhimu kwa jamii kwa kile alichokisema kuwa kinawasaidia wanaotumikia vifungo vya nje kubadili mienendo yao sambamba na kuwainua kwa miradi ya kujiendeleza kimaisha kwa kuwapa mafunzo hitajika.

Afisa huyo amewataka wakaazi wote walio na kesi mahakamani ambazo hazijatatuliwa kubeba stakabadhi hitajika ili kupata msaada wa kukamilisha kesi hizo.

Kumbu ameomba wakazi wa Mayungu na maeneo mengine kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo unaotarajiwa kuanza saa tatu asubuhi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.