KILIFI KAUNTI NI MIONGONI MWA ZILE AMBAZO ZINAKABILIWA NA UKAME

Kaunti ya Kilifi ni miongoni mwa kaunti 5 nchini ambazo zinakabiliwa na ukame mkubwa ambapo watu milioni 2 katika taifa hili wanadaiwa kuhitaji msaada wa chakula na maji.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa mpango wa kusambaza chakula na maji kwenye kaunti ambazo zimeathirika zaidi na ukame, waziri wa ugatuzi nchini Eugine Wamalwa amesema serikali imeweka mikakati thabiti ya kukabiliana na hali hiyo.
Haya yanajiri eneo bunge la Ganze kaunti ya Kilifi likiwa miongoni mwa maeneo ambayo wanyeji wameathirika zaidi na baa la njaa huku wakitaka hatua za haraka kuchukuliwa kabla ya hali kuwa mbaya zaidi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.