Kilifi | Asasi za usalama zaanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha kujitia kitanzi kwa mzee wa miaka 82

Asasi za usalama sehemu ya Mida eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi zimeanzisha uchunguzi dhidi ya kisa kimoja ambacho mzee mmoja mwenye umri wa miaka 82 amepatikana amejitia kitanzi.

Kulingana na naibu chifu wa Mida – Majaoni Renson Baya ni kuwa marehemu kwa jina Charo Nzovu Kalama amepatikana amejinyonga mita chache kutoka kwa makazi yake.

Aidha, Baya amehoji kuwa hadi kufikia sasa kiini cha mwanaume huyo kujitoa uhai hakijabainika.

Hata hivyo, amesema harakati za kamati ya usalama kuwatafuta washauri ambao watatwikwa jukumu la kutoa hamasa kwa jamii eneo hilo kufuatia ongezeko la visa vya watu kujitoa uhai maneneo hayo zimeanzishwa.

Mwili wa Marehemu unahifadhiwa katika chumba Cha kuhifadhi maiti katika hospital ya kaunti ndogo ya Malindi kaunti ya Kilifi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.