KENYA YAPATA PIGO KAMWAROR AKIJITOA KWENYE MASHINDANO YA OLIMPIKI 2020

Kenya yapata pigo baada ya mwariadha wa mbio za mita 10, 000 na bingwa wa New York Marathon Geofrey Kamworor kujitoa kwenye mashindano ya Olimpiki 2020 yanayoanza rasmi leo Ijumaa nchini Japan kufuatia jeraha la kifundo cha mguu.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 28 ni bingwa wa dunia mara tatu wa mashindano ya Half Marathon na alikuwa na nia ya kushinda medali ya mbio za mita 10, 000 baada ya kuibuka bingwa wa mbio hizo kitaifa.

Alishinda medali fedha 2015 Beijing nchini China nyuma ya Mo Farah wa Britain.

Jeraha hilo linakuja kufuatia kugongwa na pikipiki wakati wa mazoezi karibu na nyumbani kwake mwezi Juni mwaka jana.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.