Kenya yaangukia pua mikononi mwa Ghana kwenye kufuzu mashindano ya mpira wa magongo

Kenya imepata pigo katika juhudi zake za kurejea katika Olimpiki kwenye fani ya mpira wa magongo ya wanaume baada ya kulazwa 3-2 na Ghana katika mchujo wa Bara Afrika ulioanza mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini hapo jana.

Vijana wa kocha Meshack Senge, ambao waliichabanga Ghana 4-3 mara ya mwisho walipokutana katika mashindano haya mwaka 2015, walikuwa wakiongoza kwa 1-0 wakati wa mapumziko kupitia bao la Constant Wakhura lililopatikana dakika ya 28.

Ghana ilisawazisha katika robo ya tatu kupitia kwa Benjamin Kwofie kabla ya Kenya kuchukua uongozi tena kwa 2-1 katika robo ya mwisho kupitia kwa Festus Onyango dakika ya 51.

Hata hivyo, Ghana ilikuwa na mipango tofauti na kusawazisha tena kupitia kwa Akaba Elikem dakika moja baadaye na kisha kufuma wavuni bao la ushindi kupitia kwa Salya Nsalbini sekunde ya mwisho kutokana na kona fupi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.