Kenya | Vijana watakiwa kutumia teknolojia kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa serikalini

Vijana nchini wametakiwa kutumia vyema teknolojia ili kukabiliana na uhaba wa ajira katika taifa hili.

Haya ni kulingana na katibu katika wizara ya huduma za umma na jinsia, Raymond Ochieng, ambaye amewataka vijana kukumbatia ajira kupitia teknolojia ili kujikimu kimaisha badala ya kutegemea serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuwapa kazi.

Kwenye hotuba yake katika maadhimisho ya kitaifa ya siku ya vijana kaunti ya Kwale amesema hiyo ni njia mojawapo ya vijana kutumia ili kujiepusha na vishawishi vya kujiunga na makundi ya kigaidi pamoja na uraibu wa dawa za kulevya.

Kwa upande wake afisa mkuu mtendaji wa baraza la vijana katika taifa hili Roy Sasa Katelewa ametoa wito kwa vijana kuchukua mikopo katika hazina za serikali ili kuanzisha miradi mbali mbali ambayo itawafaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.