Kenya kushiriki mbio za Triathlon nchini Rwanda

Kupitia chama cha Triathlon cha Rwanda, nchi hiyo itaandaa Michuano ya kombe la Triathlon ya Afrika kwa mwaka wa pili mfululizo.

Michuano hiyo ya siku moja itafanyika Jumamosi hii, Julai 13, katika wilaya ya Rubavu.

Triathlon ni mbio zinazochanganya kuogelea, kuendesha baiskeli na kukimbia kwa mchezaji mmoja au kwa timu ya wanaume wawili au wanawake wawili.

Kwa mujibu wa waandaaji, mashindano hayo yatakuwa na kuogelea kwa mita 750, kuendesha baiskeli kilomita 20 na kukimbia kilomita 5.

Rwanda, wenyeji itatoa jumla ya wanariadha 16.

Nchi nyingine zitakazotoa washiriki ni pamoja na Burundi, Afrika Kusini, Kenya, Japan, Misri, Morocco, Poland na Uturuki.

Washindi kwa wanawake na wanaume, wataondoka na dola 500 kila mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.