KANYIRI AWATAKA WENYEJI WA KWALE KUSUSIA MIKUTANO YA SIASA

Wenyeji katika kaunti ya Kwale wametakiwa kususia mikutano ya kisiasa ili kujiepusha dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Kamishna wa kaunti ya Kwale Joseph Kanyiri amesema mikutao hiyo inazidi kuchangia katika ongezeko la ugonjwa wa Covid-19.
Kanyiri anasema kanuni za kudhibiti ugonjwa huo zinaendelea kupuuzwa na wenyeji hali ambayo inazidi kutia wasi wasi na kuwataka kuchukua tahadhari ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.
Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari Kanyiri amesema ni lazima kila mmoja awe mstari wa mbele katika kuzingatia masharti hayo bila kushurutishwa.
Haya yanajiri baada ya hospitali ya rufaa ya Msambweni kudaiwa kutokuwa na uwezo wa kushughulikia idadi kibwa ya watu ambao wameambukizwa ugonjwa wa Covid-19.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.