JOHN POMBE MAGUFULI AMEAGA DUNIA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameaga dunia.

Kifo cha Magufuli kimetangazwa rasmi Jumatano usiku na makamu wake Samia Hassan Suluhu.
Amesema kwamba rais Magufuli aliaga dunia katika hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es Salam mwendo wa saa kumi na mbili jioni saa za Afrika Mashariki kutokana na matatizo ya moyo.
Akithibitisha kifo hicho makamu wa rais Samia Suluhu amesema kwamba rais Magufuli alianza kuugua mnamo tarehe 14 mwezi Machi na kulazwa katika hospitali hiyo ambapo alifariki.
Magufuli ambaye ni rais wa tano wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania amefariki akiwa na umri wa miaka 61.
Kwa mujibu wa makamu huyo wa rais Magufuli alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari wa moyo kutoka hospitali ya Jakaya Kikwete.
Amesema kwamba Magufuli amekuwa akiugua tatizo la moyo kwa zaidi ya miaka 10 .
Makamu huyo wa rais ametangaza siku 14 za kuomboleza .
Amesema kwamba katika kipindi hicho chote bendera zote nchini humo zitapepea nusu mlingoti.
Hatahivyo kiongozi wa upinzani nchini Tanzania,Tundu Lissu ameishutumu serikali ya Tanzania kwa madai ya kuwahadaa watanzania ilhali Magufuli alifariki jumatano juma lililopita huku akidai kuwa ugonjwa wa korona ndio uliomuua rais huyo.
Tangazo la kifo chake linajiri zaidi ya wiki mbili tangu alipoonekana hadharani na kuzua uvumi kwamba alikuwa akiugua virusi vya corona.
atahivyo makamu wake aliwataka raia wa Tanzania kupuuzilia mbali uvumi huo.
Kulingana na katiba ya Tanzania, makamu wake atachukua uongozi na kuendeleza kipindi cha muda uliosalia.
Tayari baadhi ya viongozi kutoka mataifa mbali mbali wameanza kutuma risala za rambirambi kwa raia wa jamhuri ya Tanzania na familia ya Magufuli.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.