JINSIA YA KIKE YAFANYA VYEMA KWENYE MTIHANI WA KCPE 2021

Mumo Faith Kawi kutoka shule ya Msingi ya Karimaine ndiye Mwanunzi wa kwanza katika matokeo ya mtihani wa KCPE mwaka huu akiwa na  alama ya 433.

Yumbet  Nanzala kutoka shule ya msingi ya Chogoria kaunti ya Meru ameibuka wa pili akiwa na alama 432 na Muriithi Angel G 432 mtawalia.

Wanyonyi Samwel ni wa 3 akiwa na 431 pamoja na  Castrol William ambaye pia amejizolea alama ya 431.

Akitoa matokeo hayo waziri wa elimu nchini Prof. George Magoha amesema Jinsia ya kike imefanya vizuri katika mtihani huo ikilinganishwa na ile ya kiume.

Magoha amesema shule za umma zimefanya bora zaidi kuliko zile za binafsi huku matokeo bora yakirekodiwa katika masomo matano yakilinganishwa na ya mwaka jana 2020 yakiwemo hisabati na Insha ya Kingereza.

Matokeo duni yameripotiwa kwenye masomo matano ambayo ni Kingereza, Kiswahili miongoni mwa mengine huku Watahiniwa 8091 wakipata alama ya zaidi ya 400 na 282,000 wakipata zaidi ya alama 300.

Takribani watahiniwa milioni 1.7 walifanya mtihani huo mwaka huu wa 2021.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.