IHIENACHO AWAWEKA LEICESTER CITY NAFASI NZURI YA KUSHIRIKI LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA 

Kelechi Iheanacho alifunga bao maridadi na pia kutoa pasi kwa mchezaji mwenza ,walipotoka nyuma na kuicharanga Crystal Palace bao 2-1.

Wilfred Zaha aliwashangaza The Foxes na bao la mapema ,dakika 12 ya mchezo na hivyo kufikisha idadi ya mabao manne kuwafunga Leicester katika mechi nne mfululizo katika uwanja wa King Power.Kipindi cha kwanza kiliisha 1-0 kwa faida ya Palace.

Bao la kukomboa kwa Foxes lilikuja dakika tano baada ya kipindi cha kwanza kuanza pale ambapo Iheanacho alitoa pasi nyerezi kwa mchezaji mwenza , Timothy Castagne na kufanya mchezo kuwa 1-1.

Iheanacho alizidi kuwapa matumaini Leicester City alipofunga bao maridadi kunako ya 80 ya mchezo na kufikisha mabao 14 katika mechi 14
Wasiwasi wao kwamba huenda wasishiriki michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya uliisha baada ya ushindi wa jana baada ya kuwapita kwa alama tano wanaoshikilia nambari ya tano , Westham United.

Palace nao wanashikilia nambari ya 13 wakiwa mbele ya timu zinazoshuka daraja kwa alama 11.

Katika mechi yake ya 350 na Leicester City , Jamie Vardy alijaribu mara mbili kuwaeka Foxes kifua mbele lakini juhudi za mlinda lango wa Palace ,Vicente Guaita hazikumruhusu.

Bao la Zaha linakuwa la kumi kwa mchezaji huyo raia wa Ivory Coast msimu huu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.