IEBC TAITA TAVETA YATHIBITISHA KUPOKEA VIFAA VYA UPIGAJI KURA

Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kaunti ya Taita Taveta imethibitisha kuweka mikakati thabiti ya kuandaa uchaguzi wa huru baada ya kupokea vifaa vya upigaji kura.
Kulingana na maafisa wa tume hiyo, wamesema kando na kula kiapo cha wao kuandaa uchaguzi huru na waki, maandalizi ambayo yamewekwa kufikia sasa yatafanya kipute cha uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu wa 2022 kuandaliwa kwenye mazinga bora bila matatizo yoyote.
Aidha, maafisa hao wamesema vifaa vyote vya upigaji kura viko salama kwa ajili ya zoezi la upigaji kura.
Aidha, wametoa wito kwa kila mmoja kuzingatia kanuni ambazo zimewekwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika bila changamoto zozote.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.