IDADI NDOGO YASHUHUDIWA KWENYE USAJILI WA WACHEZAJI PROGRESSIVE FOOTBALL ACADEMY

Idadi ndogo ya wachezaji wanaojitokeza kwenye zoezi la usajili wa wachezaji watakaojiunga na Coast Stima inayoshiriki ligi ya kitaifa ya super – National Super League – yashuhudiwa katika siku ya kwanza ya zoezi hilo linaendelea katika dimba la Alaskan mji wa Malindi, kaunti ya Kilifi.

Akiongea na Tama La Spoti mkufunzi mkuu wa klabu Progressive FC Ellison Katana amesema kwamba alitarajia kupata idadi kubwa ya vijana wanaotafuta kusajiliwa na kuhimiza wachezaji wa kandanda kujitokeza kwa wingi kwani zoezi hilo litaendelea hadi kesho Ijumaa Julai 23 2021.

Awali Kupitia mtandao wa kijamii Progressive Football Academy waliweka wazi kuwa ndio wamiliki wapya wa klabu ya Coast Stima.

Kuhusu mechi ya Progressive FC dhidi ya Kenya Navy inayotarajiwa kuchezwa Jumamosi hii Katana ambaye hajawahi poteza mechi hata moja ya ligi hiyo amesema kwamba wamejipanga vilivyo na wako na nafasi kubwa ya kuandikisha ushindi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.