IDADI KUBWA YA WALEMAVU HAWAJAKUWA WAKIPOKEA VITAMBULISHO VYA WALEMAVU

Mwenyekiti wa walemavu katika eneo Furunzi eneo bunge la Malindi Kaunti ya Kilifi David Karisa Thoya amesema kuwa idadi kubwa ya walemavu hawajakuwa wakipokea vitambulisho vya walemavu licha ya wao kusajiliwa kama walemavu katika taasisi husika.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee na kituo hiki Karisa ametaja hatua hiyo kama mhangamoto kuu kwani baadhi ya walemavu mashinani wamekuwa wakipitia hali ngumu katika kupokea misaada kutoka kwa serikali huku akilalamikia hatua ya baadhi ya vifaa wanavyo hitaji kutowafikia walengwa mashinani.

Karisa ameeleza kuwa baadhi ya watu wanaoishi na ulemavu husalia majumbani pasi na kuwa na ufahamu wowote kuhusiana na ujio wa vitambulisho vyao katika afisi husika kufuatia hatua ya kukosa watu wa kuwasaidia kufuatilia swala hilo katika afisi hizo.

Aidha amewataka viongozi wa walemavu katika kaunti ya kilifi kutia bidii katika maswala ya kuwasaidia walevu kupata misaada hiyo kwa kile alichosema kuwa walemavu wamekuwa wakitegemea kupata msaada wa viti vya magurudumu kutoka kwa wahisani na wala sio serikali.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.