IDADI KUBWA YA VIJANA NCHINI KENYA WANAKUMBWA NA UHABA WA AJIRA

Idadi kubwa ya vijana humu nchini wanakumbwa na uhaba wa ajira hata baada ya kuhitimu katika tasnia mbalimbali.
Haya ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa muungano wa wanafunzi katika chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa, Dennis Okanga ambaye amesema kuwa mfumo unaotumika nchini unasababisha vijana wengine waliohitimu kukosa ajira.
Okanga amewakashifu wanasiasa kwa kutumia vijana kujinufaisha badala ya kuwasaidia kujiimarisha kiuchumi huku akiongeza kuwa vijana wengi wanaishia kujiingiza katika uhalifu kutokana na ukosefu wa mfumo maalum unaowawezesha kiuchumi.
Okanga ameiomba serikali kuweka mikakati thabiti ili kuhakikisha vijana hawakosi ajira baada ya kuhitimu kwa kuwa vijana wengi wanaelekea nchi za nje kutafuta ajira.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.