HUSSEIN MIJJI AWATAKA WENYEJI WA LAMU KUSHIRIKIANA

Mkurugenzi wa shirika la maendeleo la kijamii la LAMU ACTION DEVELOPMENT INITIATIVE Hussein Mijji ametaja suala la ufisaji kuwa kizingiti kikuu katika kukabiliana na ulanguzi wa dawa za kulevya kaunti ya Lamu.

Kwa mujibu wa Mijji baadhi ya maafisa wa serikali hushirikiana na walanguzi wa dawa za kulevya na kujihusisha na vita dhidi ya mihadarati.

Vilevile, amesema serikali inapaswa kubuni mbinu mwafaka za kukabiliana walanguzi wa utumizi wa dawa za kulevya.

Mijji sasa amewataka wenyeji kushirikiana na asasi husika vya usalama pamoja na zile zinazokabiliana na utumizi wa dawa za kulevya ili kukabiliana na ulanguzi huo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *