Mwaniaji wa wadhifa wa ugavana kaunti ya Kwale Profesa Hamadi Boga ameibua madai kuna njama ya muungano wa Kenya kwanza kufanyika kwa wizi wa kura kwenye kaunti hiyo.
Boga ambaye anawania wadhifa huo akitumia chama cha ODM anadai kuwa wapinzani wao wanawatumia maafisa wa serikali ya kaunti ili kutekeleza wizi huo.
Katika kikao na wanahabari, Boga ametaja hatua hiyo kuwa ukiukaji mkubwa wa sheria kwa wafanyikazi wa serikali kujihusisha na maswala ya siasa.
Ni kauli iliyoungwa mkono na kiongozi wa Azimio kaunti hiyo James Nyakiti ambaye amesisitiza kuwa tayari wapinzani wao wanawatumia maafisa hao ili kuiba kura za wadhifa wa ugavana.
HAMADI BOGA AIBUA MADAI KUHUSU NJAMA YA WIZI WA KURA KWALE
