GIDEON MOI AZURU PWANI

Seneta wa Baringo ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha KANU Gideon Moi amezuru kanda ya pwani katika harakati za kuuza azima yake ya kuwania wadhifa wa urais kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2022.
Moi ambaye amekutana na wanachama wa chama hicho cha KANU eneo la Diani kaunti ya Kwale anasema muungano wa One Kenya Alliance bado upo na wanashauriana ili kupata mgombea mmoja ambaye atapeperusha bendera ya muungano huo.
Amesema vyama vya KANU, ANC, FORD KENYA na WIPER vinashauriana na kinara wa ODM Raila Odinga ili kujiunga na muungano huo ili kukabiliana na naibu wa Rais kwenye uchaguzi huo mkuu.
Baadhi ya viongozi ambao waliandamana na Moi akiwemo mwakilishi wa kike kaunti ya Lamu Ruweida Obo, aliyekuwa mbunge wa Lamu Magharibi Julius Ndegwa na Mbunge wa Fafi Abdikarim Osman Mohamed wamempigia debe Gideon Moi kuchaguliwa kama rais wa taifa hili mwaka wa 2022.
Ni ziara ambayo inajiri baada ya mbunge wa Tiaty William Kamket kusema Gideon Moi atatangaza rasmi azima yake ya kuwania wadhifa huo tarehe 30 mwezi huu wa Septemba 2021 kwenye ukumbi wa Bomas jijini Nairobi.
leo Alhamisi Gideon Moi atakuwa katika kaunti ya Mombasa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.