Geoffrey Kamworor kuiwakilisha Kenya kwenye mbio za dunia Doha

Bingwa wa nusu marathoni duniani Geoffrey Kamworor ameamua kujitosa kwenye mbio za mita 10,000 za fainali za ubingwa wa Huduma za Polisi za Taifa zinazoanza leo huko Kasarani, Kenya.

Kamworor, ambaye anataka kuiwakilisha Kenya kwenye mbio za mabingwa wa dunia zitakazofanyika Doha mwaka huu, amesema yuko tayari kunyakua taji la Polisi kwa ushindi wake wa mara nne.

Hizi zitakuwa ni mbio zake za pili katika msimu huu.

Mshindi huyo wa mara mbili wa Nusu marathoni ya dunia na mbio za nyika alisalimisha taji lake la mbio za nyika kwa Waganda Joshua Cheptegei na Jacob Kiplimo, waliochukua medali ya dhahabu na fedha mtawalia Mach 30 nchini Denmark.

Hata hivyo Kamworor, mwenye miaka 26, alirejesha tena nguvu zake na kushinda Grand Prix mbio za maili 10 nchini Switzerland May 11.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.