Gareth Bale afungia Real bao la ushindi

Nyota Gareth Bale alitokea benchi katika kipindi cha pili na kuwafungia waajiri wake Real Madrid bao katika mchuano wa kirafiki uliowashuhudia miamba hao wa soka ya Uhispania wakizidiwa nguvu na AS Roma katika mikwaju ya penalti nchini Italia.

Bale alikuwa akirejea katika kikosi cha kwanza cha Real baada ya kusalia nje kwa muda mrefu tangu uhamisho wake kwenda timu ya Jiangsu Suning nchini China kugonga mwamba.

Mshindi wa mchuano huo aliamuliwa kwa mikwaju ya penalti baada ya pande zote mbili kuambulia sare ya 2-2 mpaka muda wa kawaida ulipotimia. Diego Perotti wa Roma na Edin Dzeko walizifuta juhudi za Marcelo na Casemiro ambao awali, walikuwa wamewaweka Real kifua mbele.

Katika penalti, Marcelo aliupoteza mkwaju wake na kuwapa Roma ushindi wa 5-4 uwanjani Olimpico.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.