FREDRICK OCHIENG KUZURU KAUNTI 25 NCHINI KUHAMASISHA WAKENYA KUHUSU UGONJWA WA COVID-19

Serikali kuu kupitia wizara ya afya nchini inapozidi kuweka mikakati ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, baadhi ya wakenya wamekuwa wakitumia mbinu mbali mbali kuwahamasisha Wakenya umuhimu wa kujilinda dhidi ya maambukizi hayo.
Fredrick Ochieng kutoka kaunti ya Marsabit amejitolea kutoa hamasa kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kuzingatia masharti hayo ya wizara ya afya ili kuzuia msambao wa virusi vya Corona kwa kuendesha baiskeli kutoka marsabit ili kufanikisha hilo.
Kwenye mahojiano ya kipekee na kituo hiki Ochieng amesema ameendesha baiskeli kutoka Marsabit hadi Tana River alikoanzia rasmi zoezi hilo tarehe 4 Mwezi huu wa Mei na anapania kuzuru kaunti 25 nchini.
Ochieng ametaja baadhi ya changamoto ambazo anakumbana nazo kwenye safari anapoendesha baiskeli wakiwemo wanyama pori.
Hata hivyo ametoa wito kwa serikali kuu na zile za kaunti kutumia vizuri fedha zinazotolewa za kukabiliana na Janga la virusi vya Corona kama inavyopaswa huku akiwashauri Wakenya kujitolea vilivyo katika kulitumikia taifa hili.
Zoezi hilo litakamilika tarehe 16 Mwezi huu wa Mei katika kaunti ya Turkana.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.