FREDRICK NGUMA ATOFAUTIANA NA LALAMA ZA WAZAZI WA KAUNTI YA KILIFI

Wazazi wanaodai kuwa baadhi ya shule kaunti ya Kilifi zinawatoza kiwango cha juu cha ada ya masomo ya ziada kwa watoto, yamepingwa na Katibu wa muungano wa KNUT tawi la Malindi na Magarini kaunti ya Kilifi Fredrick Nguma ambaye amesema pesa hizo huafikiwa baada ya makubaliano baina ya wazazi, walimu pamoja na bodi ya shule.
Nguma amesema hawafai kulalamika kwani linatokana maamuzi yao na hakuna ambaye aliwashurutisha katika ulipaji huo wa fedha za masomo ya zaida kwa watoto wao.
Kwa mujibu wa Nguma hakuna ada ya masomo ya ziada ambayo inatekelezwa bila kuwepo na makubaliano.
Aidha Nguma amewaomba wazazi kuwa makini wanapokubaliana kwenye masuala mbambali wanapofanya maamuzi na kuwataka wazazi wote kutoa maoni yao wakati wa kubuni sheria kama hizo za kulipa ada ya masomo ya ziada kwa watoto wa ili kuzuia mvutano katika ulipaji wa pesa hizo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.