FLORA CHIBULE ASEMA WAMEDHIBITI BIASHARA YA MUGUKA KAUNTI YA KILIFI

Naibu Gavana wa kaunti ya Kilifi Flora Chibule amesema biashara ya Muguka kaunti ya Kilifi imedhibitiwa vilivyo.

Kulingana na Chibule ambaye alikuwa akizungumza na mwanahabari wetu kiwango cha fedha kinachotozwa magari yanayoingiza Muguka hapa kaunti ya Kilifi ni cha juu mno hali ambayo imefanya wafanyabishara hao kushindwa kuendeleza biashara hiyo hapa Kilifi.

Chibule amesema ulaji wa Muguka umekuwa ukiwaathiri vijana wengi kiafya na hata baadhi yao kushindwa kuendeleza shughuli zao mbalimbali kutoka na hali ya kudorora kwa afya zao.

Vilevile, Chibule ameahidi kwamba serikali ya kaunti ya kaunti ya Kilifi itaendeleza harakati za kuwakabili kisheria wale ambao wanaendeleza biashara ya Muguka na dawa za kulevya.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *