FEDHA ZATENGEWA KAMATI YA MKATABA WA MAENDELEO YA JAMII

Zaidi ya shilingi milioni 200, zimetengewa kamati ya mkataba wa maendeleo ya jamii zilizoathirika na shughuli za uchimbaji madini, (CDAC) katika kaunti za Kwale na Mombasa.

Meneja msimamizi wa masuala ya jamii katika kampuni ya uchimbaji madini ya Base Titanium Pius Kassim, amesema fedha hizo ni asilimia moja ya mgao wa jamii, zilizoathirika katika kaunti hizo.

Kulingana na Kassim, fedha hizo zimetengewa maeneo ya Msambweni, Lungalunga na Likoni yaliyoathirika na uchimbaji wa madini, unaoendelezwa na kampuni hiyo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo katika eneo bunge la Msambweni Mshenga Ruga, amesema shilingi milioni 15 zitatumika kwa ufadhili wa masomo ya wanafunzi wasiojiweza katika kaunti ya Kwale.

Ruga, amesema fedha hizo zinawalenga wanafunzi 370 wa kidato cha kwanza, waliopata chini ya alama 350 na wale wa vyuo vya kiufundi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *