FAMILIA MOJA ENEO LA MTWAPA YA LALAMIKIA KUHANGAISHWA NA BWENYENYE KUFUATIA MASWALA YA UMILIKI WA ARDHI

Huku swala la ardhi likiendlea kuzua utata kati ya jamii ukanda huu wa Pwani, jamii ya marehemu Mzee Charo baya eneo la Mzambarauni mjini Mtwapa kaunti ya Kilifi, sasa imesalia pasi na maakazii baada ya bwenyenye mmoja, kudai umiliki wa ardhi yao na hata kutekeleza ubomozi, kwa ushirikiano na maafisa wa polisi eneo hilo.

Kulingana na Ismael Charo ambaye ni mwanawe marehemu ,bwenyenye huyo amekuwa akiwahangaisha, baada ya mamake kuaga dunia katika eneo hilo, licha ya wao kuishi katika kipande hicho cha ardhi kwa takriban zaidi ya miaka 70.

Aidha Charo ameelezea kuwa familia yake imeendelea kuishi kwa hofu kwani wamekuwa wakihangaishwa na maafisa wa polisi, huku wakiitaka serikali kupitia taasisi husika kuingilia kati, na kuhakikisha kuwa jamii hizo zinapata haki.

Hata hivyo wakaazi wa eneo hilo wamekata kauli ya kuto ondoka katika kipande hicho cha ardhi, licha ya kuendelea kupokea dhulma na vitisho kutoka kwa bwenyeye huyo

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.