Eliud Kipchoge kuvunja rekodi Norway

Nyota Eliud Kipchoge atawekewa kasi na ndugu watatu kutoka Norway – Henrik, Filip na Jakob Ingebrigtsen – atakapojaribu tena kuwa binadamu wa kwanza kukamilisha mbio za kilomita 42 chini ya saa 2:00:00 jijini Vienna nchini Austria mnamo Oktoba 12, 2019.

Mkenya huyo, ambaye ni bingwa wa Olimpiki na mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za kilomita 42 ya wanaume ya saa 2:01:39, alikosa kwa sekunde 25 kutimka umbali huo chini ya saa mbili mjini Monza mwezi Mei mwaka 2017.

Katika jaribio lake la kwanza mjini Monza nchini Italia, Kipchoge, 34, aliwekewa kasi na gari pamoja na wakimbiaji ili kuzuia upepo kupunguza kasi yake.

Usaidizi huo ulimaanisha kuwa muda wake wa saa 2:00:25 haukuweza kutambuliwa na Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) kama rekodi ya dunia. Rekodi yoyote itakayopatikana Vienna pia haitatambuliwa na IAAF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.