ELISHA ROTICH AONGOZA WAKENYA KUVUNJA REKODI ZA MARATHON

 

Mwanariadha wa Kenya Elisha Rotich aliibuka mshindi wa mbio za Paris marathon siku ya jana baada  kuweka rekodi mpya ya muda wa masaa 2:04:21 na kutupilia mbali rekodi iliyowekwa na Kenenisa Bekele wa Ethiopia mwaka 2014 yaa muda wa masaa 2:05:04.

Hailelmaryam Kiros wa Ethiopia alimaliza wa pili kwa muda wa masaa 2:04:42 huku Hillary Kipsambu wa Kenya akimaliza wa tatu kwa muda wa masaa 2:04:45.

Katika mbio zingine mkenya Angela Tanui aliweka rekodi mpya kwa mara ya kwanza kabisa katika mbio za Amsterdam marathon nchini Uholanzi baada ya kumaliza wa kwanza kwa muda wa masaa 2:17:57.

Mkenya mwenzake Maureen Chepkemoi alimaliza wa pili kwa muda wa masaa 2:20:18 na nafasi ya tatu kutwaliwa Na Haven Hailu wa Ethiopia kwa muda wa masaa 2:20:19 huku upande wa wanaume Kenya wakichukua nafasi ya pili.

Katika mbio za Cape town marathon, Lydia Simiyu aliibuka mshindi baada ya kukimbia kwa muda wa masaa 2:25:41. Lucy Karimi alimaliza wa pili kwa muda wa masaa 2:25:53 kabla ya Aynalem Teferi wa Ethiopia kumaliza wa tatu kwa muda wa masaa 2:26:09.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.