CHUO KIKUU CHA PWANI KINAKABILIWA NA MADAI YA ULAGHAI

Tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi nchini EACC imeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya kuwepo na ulaghai katika mchakato wa ununuzi katika chuo kikuu cha Pwani kaunti ya Kilifi.

Kulingana na barua ambayo ilitumwa kwa naibu Chansela wa chuo hicho na afisa mkuu wa upelelezi Tabu Lwanga chuo hicho kinakabiliwa na madai ya kupendelea kampuni za bima kwa kuzipa zabuni za kusajili wafanyikazi katika bima ya afya.

Katika barua hiyo Lwanga amesema madai hayo yanayokabili chuo hicho ni ya miaka mingi na kumtaka naibu Chansela wa chuo hicho kuhakikisha zabuni zote ambazo zinatolewa zinaambana na sheria.

Lwanga amesema ikiwa uchunguzi wao utabaini kuwa chuo kikuu cha Pwani kaunti ya Kilifi kilikiuka sheria kitakabiliwa na mashtaka ya uhalifu.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *